Thursday, 30 October 2014
NATURAL WHITE COMPETITION JUMAPILI HII CLUB MAISHA DAR -ES SALAAM.
NATURAL WHITE COMPETITION jumapili ndio ule usiku wa wewe mtoto wa kike kupendeza zaidi nakutumia urembo wako wa asili. Mashindano haya yameanza wiki mbili sasa wiki iliyopita ilikuwa nikumtafuta msichana mwenye uzuri wa asili ya weusi na walifanikiwa kupatikana ssa wiki hii ni mashindano yakumsaka mwanamke au binti mzuri mwenye uzuri wa asili ya weupe na wiki inayofuata baada ya hyo ni jumapili ya tar 16/11/2014 zitafanyika fainali za mashindano haya na mshindi atapata zawadi yakitita cha tsh 500,000/= laki tano taslimu za kitanzania. Kwa hiyo usikose kuhudhuria mashinadano haya na usiku huo atakayesindikiza kwa show kali ni Hemed PHD ataperform ngoma zake zote.
Tuesday, 7 October 2014
PROFFESOR JAY MWANALIZOMBE ANAVUKA MAJI HADI CLUB KAKALA KIGAMBON JUMAMOSI HII
Mwanalizombe studio inamdondosha Proffesor Jay Club kakalA jumamosi hii katika club yakijanja. Usiku huu utapambwa na Jay Chid Benz aka King kong kuanzia saa tatu usiku mpAka majogoo. JAY atapiga ngoma zake zote kali za mwanzoni mpaka hizi mpya so jukwaa siku hiyo litawaka moto.Mlangoni utalipia buku nane kwa atakae wahi kabla ya saa sita atalipia buku saba tu. Usikosee.
Friday, 3 October 2014
NICOLE FRANKLYN SARAKIKYA NDIYE REDD'S MISS TANZANIA TALENT 2014
Nicole Franklyn Sarakikya ambaye ni mwakilishi kutoka Shinyanga 2014 usiku wa kuamkia leo alifanikiwa kuwabagwa warembo wenzake 26 kati ya 30 wanao wania taji la Miss Tanzania mwaka huu na kufanikiwa kuwa mrembo wa 3 kuingia Nusu Fainali ya Mashindano hayo baada ya kutwaa taji la miss talent. Shindano hili limefanyika New Maisha Club jijini Dar es Salaam. (Picha na Pamoja Blog)
Tano bora ilikuwa hii
Ommy Dimpoz akiwa kwenye red carpet
Msami akitoa burudani ya nguvu ndani ya Maisha club jijini Dar
Thursday, 2 October 2014
TWANGA PEPETA WAFANYA SHOO YA NGUVU CLUB YA MAISHA JIJINI DAR
Waimbaji wa Twanga Pepeta wakitoa burudani kwenye shoo yao iliyofanyika club ya Maisha jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
Kiongozi na mwimbaji wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akiimba moja ya nyimbo zao kwenye shoo hiyo iliyofanyika club maisha jijini Dar.
Mwimbaji wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Msafiri Diouf akitoa burudani ya nguvu kwenye shoo iliyofanyika club maisha jijini dar.
Wacheza shoo wa Twanga Pepeta wakifanya ya kwao kwenye club ya Maisha jijini Dar.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)