Ofisa
Elimu na Huduma kwa Mlipakodi (TRA), Bw. Sebastian Mwalele akizungumza na wasanii wa Filamu na
Muziki (hawapo pichani)
WASANII mbalimbali nchini wameanza kugomea juu ya ujio wa mfumo mpya wa hakimiliki, ikiwemo ubandikaji wa stika katika kazi zao kwa madai kuwa ni chanzo cha kikubwa cha wao kuibiwa kwani gharama za stika hizo ni kubwa mno.
Wasanii hao walionekana kutokuwa na imani na Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, wakati wakipewa mafunzo yaliyotolewa na mamlaka hiyo Basata kuhusu mfumo huo mpya ambao utamuwezesha msanii kuuza kazi zake bila kuigiliwa na maharamia/wezi.
Katibu wa Chama cha Waigizaji Tanzania, Christian Kauzeni alisema kuwa mfumo wa TRA sio mbaya kwa wasanii lakini kikubwa hasa ni kwamba kodi iliyopangwa kutozwa kwa wasanii ni kubwa tofauti na mapato watakayoyapata kutokana na mauzo ya kazi zao.
Kauzeni alisema kuwa kutokana na mfumo huo kuna baadhi ya wasanii hawaelewi chochote juu ya urasimishaji wa kazi zao hivyo inahitajika elimu ya kutosha ili waweze kuwa na uelewa wa suala hilo.
Aidha Ofisa Elimu na Huduma kwa mlipakodi kutoka (TRA) Sebastian Mwalele, alifafanua jinsi mfumo huo wa ulipaji kodi kwa ajili ya stika, ambapo alisema kuwa katika kila stika moja itauzwa shilingi 7 ambapo msanii anatakiwa kununua stika mbili katika kila CD moja ambapo itakuwa jumla ni shilingi 14, na pia kabla ya kazi kuingia sokoni msanii anatakiwa kulipia shilingu 40 kwa hiyo inatakiwa shilingi 54 kwa kila kazi jambo ambalo wasanii wamelipinga.
Sebastian alisema kuwa ifikapo Juni 30 mwaka huu mfumo huu utaanza kazi na hivyo aliwashauri wasanii wote nchini ambao kazi zao tayari zipo sokoni kuanza mchakato wa kuzisajili na kama zipo mbioni kuingia sokoni basi waweze kuzifanyia usajili.
“Mfumo huu upo tayari kwani tume iliyoundwa ambayo inaongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamadunu na Michezo, Fenela Mkangala inafanya kazi kubwa kuhakikisha mfumo huu unaenda kama ulivyopangwa,” alisem

0 comments :
Post a Comment