Yakuza

Yakuza

blog

blog

EXTREAM

tangazo

tangazo

TANGAZA NASI

Sunday, 28 September 2014

DIAMOND AMNUNULIA WEMA GARI JIPYA KAMA ZAWADI YA BIRTHDAY

Jumapili ya September 28 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa mrembo aliyebeba taji la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu. katika kusheherekea siku hiyo mpenzi wake Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz alithibitisha kwa vitendo kuwa mapenzi yao bado yako imara, kwa kumnunulia zawadi ya gari jipya aina ya Nissan.
wema6
Picha ya gari hilo la rangi nyeusi iliambaatana na ujumbe mzuri ambao Diamond alimwandikia wema kupitia akaunti yake ya Instagram yenye followers 236,841.
“Nlitama nikupe vingi, wenda ingenisaidia kueleza ni kias gani napenda nikuone ukifurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa…lakini tu sina uwezo huo mumy… tafadhari pokea kidogo hichi nlichojaaliwa leo….”
wema
Mwimbaji huyo wa ‘Number’ aliitumia siku hiyo ya birthday wa Wema kusafisha tetesi zilizokuwa zimesambaa kuwa huenda wakawa wameachana, hasa baada ya magazeti ya udaku kuandika kuwa anataka kumuoa Meninah. Kabla hajapost zawadi ya birthday aliandika ujumbe huu mapema asubuhi.
“Laiti kama Maneno yangelikuwa ni sumu basi amini, Penzi letu lingekuwa lishazikwa na Kuoza…Maana sjui ni kipi hakijazungumzwa…..vya furaha, Chuki, shangwe, fitina, Vita, majungu, Misukosuko na mabalaa ya kila aina….lakini siku zote tumekuwa tukipendana na kuthaminiana kama tumeanzana jana, kwakuwa tulijua si kosa lao, ni hawajui tu niwapi tulipotokea…to the world, you may be one person…But to me, you are the world, My Beautiful World…na kama kukupenda ni uwendaazimu basi ni bora Nikabaki kwenye uchizi wangu kuliko kupata Ufahamu….i may not be physically present to stand by you while you cut your cake, but you’ll be in my thoughts the whole day! Happy birthday Darling….mmeo niko nahangaika, bt i will be coming home soon….Love you mama”
wema2

MASHINDANO UDO EAST AFRICA STREET DANCE YALIYOANDALIWA NA UDO YAFANYIKA CLUB MAISHA JIJINI DAR

 Hawa ndio walikuwa kikaangoni  siku ya jumapili hii na wawili wao wameyaaga mashindano  ya Dance yaliyoandaliwa na UDO(United Dance Orgarnisation) yaliyofanyika k Club ya Maisha   jijini Dar.
  Mc wa mashindano ya Dance, Gillah "The Boss" akifanya ya kwake kwenye stage ya New Maisha Club jijini Dar. 
 Mc wa mashindano ya Dance, Jillah "The Boss" akiwa na Mc Kim wakifanya ya kwao kwenye stage ya Maisha Club ya jijini Dar.
Hawa ndio walioingia kwenye kikaango wiki iliyopita 
Huyu aliyeshika Mic ndiye aliyeaga mashinda katika mashindano hayo
Mc Kim akiwaonesha madansa walioingia kikaangoni 
Jaji Steve(aliyeshika Mic)  akizungumza jambo kwenye shindano  hilo
 Jaji Joan(katikati) akizungumza jambo kwenye mashindano hayo wa kwanza kushoto  ni Chief Jaji Idrisa pamoja na jaji
 Chief Jaji Idrisa akizungumza jambo kwenye mashindano ya Street Dance Champion yaliyofanyika kwenye Club ya Maisha jiji Dar, Kulia ni Jaji Joan

Saturday, 27 September 2014

REDDS MISS TANZANIA TALENT 2014 NDANI YA NEW MAISHA CLUB DAR-ES-SALAAM.

Redds Miss Tanzania Talent inafanyika New Maisha Club Dar tar 03/09/2014. Kutakuwa na mamiss 32 watakaochuana vikali katika jukwaa la New Maisha Club. Miss wote wataonyeshana uwezo usiku huo. Msanii Omy Dimpoz atawasindikiza warembo hawa kwa kupiga show kali kama zawadi ya mashabiki zake. Mlangoni utalipia tsh 15,000/= na tshs 30000 kwa Maisha Lounge. Usiku huo utakuwa na suprise kibao kwa wewe mpenda burudani.

Thursday, 25 September 2014

TWANGA PEPETA WAFANYA SHOO YA NGUVU KWENYE CLUB YA MAISHA JIJINI DAR

 Kiongozi na mwimbaji  wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Luiza Mbutu (wa pili kutoka kulia), akiwa na Kalala Junior (wa pili kutoka kushoto) pamoja na  Haji Ramadhani (wa kwanza kulia) wakitoa burudani kwa mashabiki wao kwenye shoo iliyofanyika club ya Maisha jijini Dar
 Waimbaji wa Twanga Pepeta wakitoa burudani kwenye shoo iliyofanyika kwenye club ya Maisha jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
  Kiongozi na mwimbaji  wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akicheza moja ya nyimbo zao kwenye shoo hiyo.
 Wacheza shoo wa Twanga Pepeta wakifanya ya kwao kwenye club ya Maisha jijini Dar.
Wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja

Tuesday, 23 September 2014

TOKA CHEMSHA BONGO MPAKA SASA DADDY PROFFESOR JAY ANASHINE KAACHIA NGOMA MPYA MBILI DOUBLE CHAFU 3 NA KIPI SIJASIKIA.

Proffesor Jay msanii mwenye A.K.A nyingi sana kutokana na ukubwa wake katika sanaa toka mwaka 1980 mpaka sasa anashine tu. Proffesor Jay ni msanii mkubwa mwenye nguvu zaidi katika hii sanaa ya Muziki wa kizazi kipya. Jay ni mtu ambaye alisimamisha huu Muziki wa Bongo Flava kuwa hapa ulipo kuwepo. Muziki huu Dady ndio kautambulisha sana katika jamii hii ya Tanzania.Proffessor jay A.kA Jay wamitulinga,Jay Tunakuzimia,Nigga Jay, na Majina mengine kibao alipewa katika harakati za Muziki wa BOngo Flavour,.nIGGA jay kaachia ngoma mpya mbili kwa mpigo Chafu 3, na kipi sijasikia na hizi zote zina video zake tayari soon tu zinakuwa hewani....Stay Tune

Saturday, 20 September 2014

PEACE ONE DAY CONCERT THIS SUNDAY AT NEW MAISHA CLUB DAR ES SALAAM .

Peace One Day ni siku ya Amani Duniani siku hii inaadhimishwa Jumapili hii tar 21/09/2014 New Maisha Club Dar es salaam  onyesha hili litasindikizwa na wasanii wa kizazi kipya kama Banana zorro, Barnaba, khadija, Toto the bingwa, Q-jay kwa mara ya kwanza tokea aokoke na Alice maadhimisho haya   yataanza saa tatu usiku mlangoni utalipia tsh 10,000/=tu. Njoo ushuhudie usiku huu na njoo tuhamasishe amani Duniani.

Friday, 19 September 2014

MWANAMUZIKI WA BONGO FLAVOUR TANZANIA JUMA JUX HIVI KARIBUNI KAACHIA WIMBO MPYA UNAOKWENDA KWA JINA LA SISKII.


Mwanamuziki wa kizazi kipya Juma Jux ameamua kuachia wimbo wake mpya baada yakuacha nyimbo zake zilizotangulia kufanya vizuri katika chart zote East Afrika na Dunia nzima kwa ujumla. Juma Jux alisema kuwa wimbo mpya anaouachia umeandikwa na Mwanmuziki anaekwenda kwa jina la Mabeste pia Bongo Flava artist na kumpatia Juma Jux aufanyie kazi yaani afanye recording na kuupeleka hewani wimbo huu Umerekodiwa na mtayarishaji Maneke wa AM.RECORDS na umeshasamabazwa vituo vyote vya Radio hapa Tanzania na katika mitandao yakaijamii pia. Hivyo tembelea mitandao yote wimbo huu unapatikana. Pia endelea kusubiri hivi karibuni video ya wimbo huu utakamilika ...Thanx

REFIX YA MIRROR26 INAACHIWA IJUMAA YA LEO XXL YA CLOUDS [PREMIERES FRIDAY 19/09/2014 ON CLOUDS FM XXL 1500HRS THE REFIX]

Premieres Friday 19/09/2014 on Clouds Fm xxl 1500hrs The Refix ya Mirror itakuwa hewani muda huo ukifika hii kitu kaitengeneza Producer Lamar kutoka Fish Crubs kaa tayari kuiskia na kuipokea na kuisupport pia. MIrror na Producer  Lamar wote sio watu wakubahatisha ni watu ambao wanafanya nini katika hii sanaa ya Muziki wa Bongo Flavour.

DUNIA NZIMA INAMTAKIA SIKU YA KUZALIWA DJCHOKA MR APPETITE [HAPPY BIRTHDAY DJCHOKA]

Dj Choka Mr Appetite amezaliwa siku ya Ijumaa tar  19/09 kama hii jamaa anatimiza miaka mingi sana sababu sasa ni Baba wa Familia.Jumapili ya tar 21/092014 Dj Choka Mr Appetite anawaarika Watanzania wote pale Ten Lounge muweze kula Bata pamoja na kusheherekea siku yake yaku zaliwa.Jumapili pale Ten LOUNGE kutakuwa na celebrates wote unaowajua wewe so usikose kuja kumsupport DJchoka Mr Appetite siku yake ya kuzaliwa.

IJUMAA HII NI USIKU WA MAYENU USIKU HUU UNAFANYIKA NEW MAISHA CLUB DAR- ES -SALAAM

Ijumaa hii Club Maisha Dar es salaam ni Usiku wa Mayenu njoo ufurahie masebene na uzungushe kiuno na watoto wazuri usiku huu utalipia tshs 10,000/= tu. Bolingo zitapigwa sana na Dvj ommy crayze, dvj Ali b,Dj suma, Dj moe, na Dj jimmy, usiku huu utapambwa na hyperman hk kwa hyping za kinyama sana utapata kusikia nyimbo zote za zamani na sasa so usikose kuja New Maisha Club.

Tuesday, 16 September 2014

BAADA YA BANG BANG FT TID MZEE KIGOGO SASA TUNAJIPANGA UPYA KUACHIA NGOMA NYINGINE YAKUZAMOB4EVER.

Yakuzamob4ever walisema hivi baada ya kutoa ngoma waliomshirikisha TID na NAY WAMAITEGO sasa wanajipanga na soon tu watadondosha mzigo mpya walisema vitu vingi sana ambavyo wao wanajua tofauti na wao kuachia ngoma mpya kwanza hawa jamaa wao niwaandaaji wazuri sana wamatamasha ya nje na ndani pia wao ni Managers wa club zinaongelewa hapa Tanzania kwa mfano Geoffrey Gilla ni Marketing Manager wa New Maisha Club  Dar-es-salaam na Mbwana Khamisi ni Marketing Manager wa Club Kakala iliyopo kigamboni waliendelea kusema wao wanavipaji vingi sana na wana proffessional ya vitu vingi sana na chochote utakachowaambia wafanye wao hufanya sababu ni wajasilia mali tosha.


Yakuzamob4ever wanatokea mkoani Morogoro huko ndipo walipo anza mambo yao ya sanaa huwa wanapena sana kujifunza ndio maana wamefika hapo walipofikana wanaendelea mbele. Yakuzamob4ever ni kundi linaundwa watu wawili [Mbwana Khamisi na Geoffrey Gilla] watu hufikiria ni ndugu hapana hawa jamaa ni marafiki wamaisha yakawaida na sanaa.

Tofauti na music hawa jamaa ni Mabaharia[Seaman] Chuo walichosema haya mambo ni DMI hupenda kujifunza vitu lakini sio vitu vibay ambavyo havijengi na havimjengi mtu yoyote katiaka Maisha ya kawaida na kisanii pia.

                                     UKITAKA KUJUA MENGI KUHUSU ENDELEA KUIFUTILIA HII KURASA ....www.yakuzamob4ever.blogspot.com

USIKU WA DERA NDANI YA NEW MAISHA CLUB DAR-ES-SALAAM KILA JUMATANO.

Kila jumatano ni Usiku wa Dera club Maisha Dar-es-salaam njoo ukiwa umevali Dera kali ili upate zawadi kutoka Ndio Fashion Kinondoni kwa kawaida mlangoni utalipia tsh 10,000/= na usiku huu watoto wakike hukatika sana viuno katika mapigo ya ngoma za Kibaokata mapigo ya asili ni mapigo mazuri njoo jumatano na kila jumatano usikose.

Sunday, 7 September 2014

MASHINDANO YA DANCE YALIYOANDALIWA NA UDO YAFANYIKA KWENYE CLUB YA MAISHA JIJINI DAR

 Ton Dougue(katikati) akicheza  wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Dance yaliyoandaliwa na UDO(United Dance Orgarnisation) yaliyofanyika kwenye club ya Maisha Club ya jijini Dar.
 Mc wa mashindano ya Dance, Jillah "The Boss" akifanya ya kwake kwenye stage ya Maisha Club ya jijini Dar. 
 Chief Jaji Idrisa akizungumza jambo kwenye mashindano ya Street Dance Champion yaliyofanyika kwenye Club ya Maisha jiji Dar, Kulia ni Jaji Joan

Jaji Joan akizungumza jambo kwenye mashindano hayo
 



  
  




  


 Picha za juu zinaonesha baadi ya makundi yaliyoshiriki kwenye mashindano ya Streen Dar
Gilla(aliyeshika Mike) akiwa na baadhi washiriki la Street Dance Champions.
  Msanii wa  muziki wa kizazi kipya, Buibui akiwapagawisha mashabiki wake kwenye mashindano ya Dance yaliyoandaliwa na UDO(United Dance Orgarnisation) yaliyofanyika kwenye club ya Maisha Club ya jijini Dar.